DAR ES SALAM.

Wanawake Nchini wametakiwa kuenzi na kuunga mkono kazi zinazofanywa na Viongozi Wanawake kwenye ngazi mbalimbali za Kisiasa.

Hayo yamesemwa na Mnajimu na Mtabiri maarufu nchini Sheikh Sharifu Majini alipozungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake Mabibo Jijini Dar es Salaam alipovipongeza vyama vya Siasa vilivyowasimamisha Wanawake kwenye nafasi za Urais na Makamu wa Rais katika uchaguzi Mkuu wa mwezi Octoba 2020.

Shekhe Sharifu Majini amesema kuwa vyama vya Siasa vitambuwe kuwa kuna jamii kubwa ya Wanawake nchini ambayo wanafarijika sana kuona wanawake wenzao wanapewa nafasi ya kugombea nafasi hizo.

Akiongelea vyama vilivyowateua wanawake katika Uchaguzi Mkuu wa October amekitaja Chama cha Union for Multipart Demokracy (UMD), Sauti ya Umma (SAU), Alliance Democratic Change (ADC), Demokrasia Makini, na Chama cha Mapinduzi (CCM).

“Vyama ambavyo vimewapa fursa wakina Mama watapata kura nyingi za wananchi kutokana na hatua za vyama vyao kuwateua wakina Mama Kama wagombea mwenza na ngazi ya Urais” Amsema Sheikh Sharif.

Aidha Amesema kuwa ni vema mwanamke akathaminiwa kutokana na ushawishi wake kutokana na maendeleo anayoyaleta katika ngazi ya familia na Taifa kwa ujumla.

Akizungumzia Chama cha Mapinduzi (CCM) kumpitisha tena Mama Samia Suluhu Hassan kuwa Mgombea mweza wa Chama hicho,  Sheikh Sharif Majini amesema kuwa amefarijika sana kwa Chama hicho kumchagua tena Mama Samia kuwa Mgombea mwenza kutokana na weledi wake katika kusimamia majukumu yake.

“Huyu mama amefanya kazi kubwa kutetea maslahi ya wanawake hususani ni wale wanaoishi vijijini kwa kuwatetea kwenye nyanja mbalimbali za kiuchumi na kimaendeleo kwa ujumla”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *