Neno kigugumizi limetokana na kitenzi kugugumia ambayo ni shida ya baadhi ya watu katika kusema na inakadiriwa asilimia 5-6 inawapata watoto huku asilimia moja ikiwapata watu wazima, wanaume wanapatwa mara nne kuliko wanawake. Kwa kiingereza kigugumizi kinajulikana ‘stammer’.

Kuna vigugumizi vya aina nyingi, kuna kusimama, kusema kitu tofauti na ulichokusudia, kusita na kuhangaika kwenye kutafuta maneno ya kusema na mengineyo

Mwanasaikolojia Salahudeen Kimangale amesema kigugumizi hakina sababu moja ya kwanini mtu anakipata. Zipo sababu za kibaiolojia, kijamii na kisaikolojia.

Sababu za kibaiolojia hasa ni urithi kwa kubeba ‘genes’ kutoka kwa mzazi kuja kwa mtoto hivyo katika familia ambazo ina mtu ana kigugumizi uwezekano wa mtu kubeba hilo tatizo la kigugumizi unakuwepo.

Pia kuna tatizo la mazingira ambapo mtoto kwa sababu flani flani akachelewa kujifunza matamshi au akachelewa kupata lugha mfano kwenye maeneo yenye vita watoto wengi wanaweza kupata kwa sababu uzungumzaji unahusika na ubongo hivyo ukiona mtu anazungumza taratibu maana yake pia ubongo una’process’ taratibu. Kwenye mazingira hatarishi kama ya vita, watoto wadogo wanapokuwa wanakuwa kunakuwepo uwezekano huo.

Ally Abdallah kutoka chama cha mitindo maalum ya uzungumzaji Tanzania amesema siku hii inaadhimishwa ili na watu ambao wanacho kigugumizi kwa sababu kwa mazoea watu wenye kigugumizi wananyamazishwa na kuwa wakimya na ni kama siku ya subra kwamba watu wanaowazunguka wenye kigugumizi waweze kuwasubiri wakati wanaongea.

Watu wanadhani mtu mwenye kigugumizi ni ana ukosefu wa akili, ndio maana kwenye chama chetu hatutumii neno kigugumizi kwa sababu neno hilo limeharibiwa tunatumia neno mtindo maalum wa uzungumzaji” Ally Abdallah, Mkurugenzi Mtendaji CHAMMUTA

Dunia inavyokwenda watu wenye kigugumizi tuna Mazingira magumu sana, unazungumza na mtu ambaye hana subra hawataki kutuacha tumalize kuzungumza, wanatukatisha” Ally Abdallah, Mkurugenzi Mtendaji CHAMMUTA

Kigugumizi sio ugonjwa, wapo wanaosema watu huzaliwa hivyo hususani wakati wa utoto hiyo hali ya kigugumizi hutokea na wengine husema mtoto anaweza kumwona mtu mwenye kigugumizi naye akaiga, vyote vipo kwenye utafiti lakini hakuna uhakika kama vina ukweli” Ally Abdallah

Usimkatishe mwenye kigugumizi anapoongea, unammaliza kabisa, msubirie hadi amalize sentensi yake” Ally Abdallah, Mkurugenzi Mtendaji CHAMMUTA

Dunia inavyokwenda watu wenye kigugumizi tuna mazingira magumu sana, unazungumza na mtu ambaye hana subira hawataki kutuacha tumalize kuzungumza, wanatukatisha” Ally Abdallah, Mkurugenzi Mtendaji CHAMMUTA

Watu wanadhani mtu mwenye kigugumizi ni ana ukosefu wa akili, ndio maana kwenye chama chetu hatutumii neno kigugumizi kwa sababu neno hilo limehaharibiwa tunatumia neno mtindo maalum wa uzungumzaji” Ally Abdallah, Mkurugenzi Mtendaji CHAMMUTA

Nilipotimiza miaka mitano nilipata msiba wa baba yangu, baada ya miezi michache nilipata kigugumizi kwa mujibu wa mama alivyoniambia, kesi yangu wanasema ni mshtuko” – Ally Abdallah, Mkurugenzi Mtendaji CHAMMUTA

Kigugumizi sio ugonjwa wapo wanaosema watu huzaliwa hivyo hususani wakati wa utoto hiyo hali ya kigugumizi hutokea na wengine husema mtoto anaweza kumwona mtu mwenye kigugumizi naye akaiga, vyote vipo kwenye utafiti hakuna uhakika kama vina ukweli” Ally Abdallah

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *